Mkongwe wa ‘Rock n Roll’ Chuck Berry afariki dunia

0

Mwanamuziki mahiri wa muziki wa ‘Rock n Roll’ nchini Marekani Chuck Berry amefariki dunia nyumbani kwake Wentzville akiwa na umri wa miaka 90.

Taarifa ya Polisi katika jimbo la Missouri imesema Berry alikutwa akiwa amepoteza fahamu muda wa mchana na kukimbizwa hospitali, ambako jitihada za madaktari kuokoa uhai wake zilishindikana.

Chuck Berry amekuwa katika tasnia ya muziki huo kwa takriban miongo saba, ambapo alitunga na kurekodi nyimbo kadhaa zilizotia fora ikiwemo vibao kama ‘Roll Over Beethoven’ na ‘Johnny B. Goode’.

Tayari watu mbalimbali maarufu duniani na katika tasnia hiyo wameanza kutoa salamu zao za rambirambi, akiwemo rais mstaafu wa marekani Bill Clinton, wanamuziki Mick Jagger na Bruce Springsteen na kundi la The Jacksons.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here