Coolio kupanda jukwaani bila ‘bling-bling’ kukwepa vibaka Uingereza

0

Rapa mkongwe wa Marekani Coolio amesema anakusudia kuvua viatu vyake, mikufu na vitu vya thamani anavyovaa kabla ya kujichanganya na mashabiki wake wa Uingereza katika maonyesho yake yatakayo fanyika hivi karibuni.

Hiyo inatokana na rapa huyp kuibiwa vitu kadhaa alipofanya onyesho katika ziara yake iliyopita.

Coolio anatarajiwa kufanya maonyesho katika miji ya London, Liverpool, Birmingham, Belfast na Glasgow, ikiwa ni katika kuhamasisha ziara yake ya kimuziki ijulikanayo kama ‘I Love The 90s’.

Coolio alikumbwa na zahma la kuibiwa viatu na vitu hivyo baada ya kujirusha kwa mashabiki katika onyesho lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Staffordshire mwaka 2009.

Amesema anawachukulia mashabiki wake wa Uingereza kama marafiki  zake na wasanii wa huko kama sehemu ya familia.

Coolio alitamba katika medani ya muziki wa kufoka-foka haswa vibao vyake vya ‘Gangsta’s Paradise’ na ’C U When U Get There’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here