PICHA: Wewe unadhani huyu ana miaka mingapi?

0

TAFADHALI kutana na Lee Su Jin, daktari wa meno kutoka Korea ya Kusini. Unamuonaje  pasishaka kama mimi nilivyomuona bomba nawe unamuona hivyo hivyo na unaweza kusema ni kabinti ka miaka 20 tu! Umechemka!

Mdada huyu anayeonekana mrembo wa haja ana miaka 48 lakini kijana kwelikweli na amekuwa akifanyakazi za uganga wa meno kwa miaka 16 sasa.

Lee sasa yupo Instagram amemua kuingia katika sosho midia (@sjeuro/Instagram) hiyo ili aweze kuzungumza na watu mbalimbali.

Amesema amekuwa akikosa watu wa kuzungumza nao baada ya binti yake pekee kuacha kufanya hivyo alipoingia shule za kati.

Anasema sasa akiwa na  maelfu ya watu wanaomfuatia anajisikia raha ya kuzungumza, anajisikia raha ya kutakwa kuzungumza na ndicho anachotaka!.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here