ESRF yaanda majadiliano kuhusu ukuaji wa miji nchini

0

Imeelezwa kuwa Tanzania inatakiwa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha miji yote inapangwa kulingana na ukuaji ili kumaliza changamoto zote zinazokabili miji hiyo na hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchumi wakati.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida katika majadiliano yaliyoandaliwa na ESRF kuhusu ukuaji wa miji nchini na hatua zinatotakiwa kuchukuliwa.

Dk. Kida alisema kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu kwenye miji mbalimbali nchini jambo ambalo miji mingi haikuwa imejipanga kukabiliana nalo na hivyo limekuwa likisababisha kutokea changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa watu wa eneo husika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho katika majadiliano yaliyoandaliwa na ESRF kuhusu hali ukuaji wa miji nchini.

“Tumekuwa na wadau tukianzisha majadiliano kuhusu ukuaji wa miji kama mnavyojua miji yetu inakua na tunatarajia ifikapo mwaka 2040 Watanzania zaidi ya nusu watakuwa wanakaa mijini hivyo ni muhimu kuanza kufikiria jinsi gani tunaweza kuboresha miji na makazi,” alisema Dk. Kida.

Alisema kupitia tafiti ambazo ESRF inazifanya zinaweza kutumiwa na serikali kukabiliana na changamoto hizo zinazokabili miji mingi nchini.

“Kwa hali ya mipango miji kuna changamoto hasa katika huduma kama nishati, huduma za kijamii na hata ajira kwa vijana wetu walio mijini kwa hiyo kuna makusudi kabisa kufanya mikakati kupitia tafiti zetu kuona jinsi gani tunaweza kushauri miji yetu,” alisema Dk. Kida.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Maduka Kessy akifungua majadiliano yaliyoandaliwa na ESRF kuhusu hali ya mipango miji nchini.

Naye mgeni rasmi katika majidiliano hayo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Maduka Kessy alisema Serikali inafahamu ni jinsi gani miji mingi imekuwa na changamoto na tayari imeanza kuchukua hatua.

Kessy alisema Serikali imechagua mikoa minne ambayo itaanza nayo kuipanga ili kuona namna gani inaweza kumaliza matatizo ambayo inawakabili na baada ya hapo itaendelea na miji mingine.

Kate Owens kutoka World Resources Institute akielezea jinsi hali ya mipango miji ilivyo nichini katika majadiliano yaliyoandaliwa na ESRF kuhusu hali ya mipango miji nchini.

“Miji inakua bila viwanda bila ajira na hasa kwa vijana na tukiendelea hivi inatupa changamoto jinsi ya kufika huko kwenye uchumi wa kati, lazima tuweke majadiliano ya wazi katika miji yetu na tuone jinsi gani tunatoa ajira na hivyo kutoa huduma kwa urahisi kwa jamii,

“Kwa upande wa Serikali katika mpango wa miaka mitano ambao unaendelea unatekelezwa tumeainisha lazima tuanze kupanga miji, tumeanza na miji minne na inaweza kufika sita, kwa sasa ni Dar, Dodoma, Arusha, Mwanza na inaweza kuongezeka Mtwara na Mbeya,” alisema Kessy.

Anton Cartwright kutoka Africa Centre for Cities (ACC) akielezea hatua za kuchukua kupanga miji katika majadiliano yaliyoandaliwa na ESRF kuhusu hali ya ukuaji wa miji nchini.
Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wa majadiliano kuhusu hali ya ukuaji wa miji nchini wakichangia mada zilizowashilishwa katika majadiliano hayo.

Picha juu na chini ni baadhi ya washiriki wa majadiliano hayo yaliyoandaliwa ya hali ya ukuaji wa miji nchini.

Washiriki wa majadiliano ya hali ya ukuaji wa miji nchini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika majidiliano hayo yaliyohusisha wadau kutoka sehemu mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here