Beckham ageukia filamu, aonekana kuchemsha!

0

Mchezaji maarufu wa soka duniani David Beckham amewaacha hoi mashabiki wake, baada ya kuigiza katika filamu mpya inayoandaliwa na muongozaji Guy Ritchie.

Filamu hiyo ambayo bado haijaachiwa rasmi, Beckham ameigiza kama shujaa wa Cockney mwenye kinyongo anayeitwa ‘Trigger’.

Baada ya trela mpya ya filamu hiyo iitwayo ‘King Arthur: Legend of the Sword’ kutolewa, wengi kati ya mashabiki wake wameonekana kutoridhishwa na kiwango cha uigizaji kilichoonyeshwa na Beckham.

Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 42, katika filamu hiyo pia ameigiza na wacheza sinema Jude law na Erick Bana, ambapo inatarajiwa kuonyeshwa rasmi katika majumba ya sinema nchini Uingereza mnamo Mei 19 mwaka huu.

Hata hivyo watazamaji wengi walioiona trela hiyo wametoa maoni yao katika mitandao na kumlaumu muongozaji Guy Ritchie kwa kumshirikisha Beckham ambaye ni rafiki yake wa karibu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here