Mastaa Ben Affleck na Jennifer Garner wapigania ndoa yao waahirisha shauri la talaka

0

BAADA ya kukaa kwa miaka 11 na kisha  kutaka kuachana  mastaa wawili wa Hollywood,Ben Affleck na Jennifer Garner  wamesema hebu subiri katika shauri lao la ndoa wakiamini kwamba wanaweza kumalizana na wakaendelea na ndoa yao.

Habari zinasema kwamba wawili hao wameona kwamba wanaweza kupambana kuokoa ndoa yao pamoja na kwamba miaka ya karibuni Ben alishikwa ugoni na mkewe kwa kutembea na mdada wa kike anayewasaidia nyumbani.

“Hakika anataka kurekebisha mambo na Ben wake. Wanaipa ndoa yao pumzi nyingine ya uhai,” habari  za kuaminika kutoka kwa rafiki wa karibu na Garner amesema.

Akizungumza na jarida la People alisema wawili hao bado wanapendana na wanawapenda watoto wao na watoto wanawapenda wazazi kwa hiyo wanajaribu tena.

Akizungumza hali halisi ya ndoa hiyo, jirani huyo amesema kwamba si rahisi ni ngumu lakini wanajaribu.

Habari zinasema kwamba Garner na Affleck,wote wakiwa 44, bado wanaishi pamoja licha ya kutangaza kwamba wanataka kutalikiana Juni 2015.

Taarifa hizo ambazo zilitokea wakati kashifa ya Ben ya kutembea na msaidizi wa ndani, Christine Ouzou­nian inaunguruma zimeelezwa kuwa sio sababu ya wawili hao kutaka kutengana.

“Ngoja niwaambieni suala la kutengana ni la muda mrefu kabla sijasikia suala la  Ben kutembea na msaidi wa ndani,”  alisema wakati akizungumza na Vanity Fair mwaka jana.

Garner amekuwa akiihami sana ndoa yake na kusema kwamba ilikuwa ndoa ya kweli na wala haikuwa ndoa ya kutaka picha zipigwe na hivyo kwake yeye usalama wa ndoa yake na uwajibikaji ni muhimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here